1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund yatinga robo fainali za Champions

Lilian Mtono
14 Machi 2024

Borrusia Dortmund imefanikiwa kuingia kwenye hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2021 baada ya kuichapa PSV Eindhoven mabao 2-0.

https://p.dw.com/p/4dUPD
Ligi ya Mabingwa | Borussia Dortmund - PSV Eindhoven
Wachezaji wa Borussia Dortmund wakishangilia baada ya Jadon Sancho kufunga bao na kuisaidia timu yake kusonga mbele kwenye michuano ya Champions dhidi ya PSVPicha: Thilo Schmuelgen/REUTERS

Mabao ya Borussia Dortmund yalifungwa na Jadon Sacho na Marco Reus.

Dortmund ilitoka sare ya bao 1-1 walipokutana mara ya kwanza nchini Uholanzi mwezi uliopita na ushindi huu wa leo, unaifanya timu hiyo kuwa na jumla ya mabao 3-1.

Kocha wa Dortmund Edin Terzic amesifu mchezo aliouonyesha Sancho. "Nimefurahi kwamba Sancho amefunga goli. Amecheza vizuri sana," aliwaambia waandishi wa habari.  

"Nadhani kwamba leo Jadon ametuonyesha kiwango chake cha juu kabisa tangu aliporudi kwetu."

Atletico Madrid nayo imeiondoa Inter Milan kwa jumla ya mikwaju ya penati 3-2.

Timu nane zinazokutana kwenye robo fainali Atletico, Dortmund, Bayern Munich, PSG, Real Madrid, Manchester City, Arsenal na  Barcelona.