1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Dortmund kukosa wachezaji kadhaa dhidi ya Bayern Munich

21 Aprili 2022

Borussia Dortmund inakumbwa na msururu wa majeruhi kuelekea kwa mechi muhimu ya Jumamosi hii dhidi ya mabingwa watetezi Bayern Munich, mechi ambayo inaweza kuipatia Bayern Munich taji lake la 10 mfululizo la Bundesliga.

https://p.dw.com/p/4AFOT
Fußball Bundesliga | Dortmund - Wolfsburg
Picha: Ina Fassbender/AFP/Getty Images

Kocha wa Dortmund Marco Rose amesema mlinda lango Gregor Kobel amepata jeraha wakati alipokuwa akifanya mazoezi, na atakuwa nje kwa wiki moja au zaidi.

Giovanni Reyna na Thomas Meunier wana majeraha ya muda mrefu huku kiungo Axel Witsel, Mats Hummels, Donyell Malen, Mahmoud Dahoud na Thorgan Hazard pia wanauguza majeraha.

Aidha kuna mashaka kuhusu uwepo wa Dan-Axel Zagadou na Marius Wolf.

Dortmund inayoshika nafasi ya pili, iko alama tisa nyuma ya viongozI Bayern Munich zikiwa zimesalia mechi nne tu kabla ya kukamilika kwa ligi kuu ya Bundesliga msimu huu ikimaanisha kuwa, ushindi wa Bayern katika uwanja wao wa nyumbani wa Allianz kutaithibitishia ubingwa.

"Bayern inaweza kuwa bingwa Jumamosi na watacheza kwa ari kubwa,” amesema Rose. "Tunataka kuzuiwa hilo. Tulikuwa na mchezo mzuri wikendi iliyopita dhidi ya Wolfsburg, tunahitaji kucheza kama tulivyocheza na Wolfsburg au hata kuongeza kiwango kwa dakika 90.”