1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

DeSanris ajiondowa kuwania uteuzi Republican

Mohammed Khelef
22 Januari 2024

Gavana wa Florida Ron DeSantis amejiondoa kwenye kinyang'anyiro cha urais na kutangaza kumuunga mkono Donald Trump.

https://p.dw.com/p/4bWso
USA | Iowa Caucus | Ron DeSantis
Gavana Ron DeSantis wa Florida.Picha: Anna Moneymaker/AFP/Getty Images

DeSantis anachukua hatua hiyo siku mbili tu kabla ya kura ya mchujo katika Jimbo muhimu la New Hampshire na chini ya wiki moja baada ya kushindwa vibaya kwenye jimbo la Iowa.

SB: DeSantis: Sikuwa nakubaliana na Donald Trump, katika masuala kama vile janga la UVIKO-19 na namna alivyomsifia Anthony Fauci. Trump ni bora kuliko rais wa sasa, Joe Biden.

Hilo liko wazi. Nimetia saini ahadi ya kumuunga mkono mgombea wa chama cha Republican na nitaheshimu ahadi hiyo. 

DeSantis aliyechukuliwa na Republican kama mbadala wa Trump kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Novemba, anaacha mnyukano mkali kati ya Trump na aliyewahi kuwa balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Nikki Haley.