1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaChina

China na Marekani kuanza tena mazungumzo ya kijeshi

Tatu Karema
16 Novemba 2023

Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Marekani Joe Biden wamekubaliana kudumisha kiwango fulani cha mazungumzo ya kijeshi kati ya mataifa hayo mawili kwa misingi ya usawa na heshima

https://p.dw.com/p/4Yr91
Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia) na mwenzake wa China Xi Jinping wakutana pembezoni mwa mkutano wa APEC mjini San Fransisco Novemba 15, 2023
Rais wa Marekani Joe Biden (Kulia) na mwenzake wa China Xi JinpingPicha: Doug Mills/AP Photo/picture alliance

Viongozi hao wawili wamekutana kwa masaa kadhaa pembezoni mwa mkutano wa kilele wa Ushirikiano wa Kiuchumi wa nchi za Asia na Pasifiki, APEC, mjini San Fransisco nchini Marekani.

Xi na Biden waahidi ushirikiano zaidi kati ya mataifa yao

Wawili hao waliahidi ushirikiano utakazozileta karibu China na Marekani katika kurejelea mazungumzo ya kawaida chini ya kile kinachojulikana kama mkataba wa ushauri wa kijeshi wa Bahari ambao hadi mwaka 2020 ulikuwa umetumika kuboresha usalama angani na baharini.

Soma pia: Xi na Biden wawasili San Francisco kwa mazungumzo muhimu

Baada ya mkutano huo kukamilika, afisa mmoja mkuu wa Marekani aliyezungumza kwa sharti la kutotambulishwa, alisema kuwa makubaliano hayo ya kijeshi yanamaansiha kuwa waziri wa ulinzi wa Marekani Lloyd Austin sasa anaweza kukutana na mwenzake wa China pindi atakapochaguliwa.