1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Blinken kwenda Saudi Arabia wiki ijayo

3 Juni 2023

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken anatarajiwa kufanya ziara nchini Saudi Arabia juma lijalo, katika kipindi hiki kukiwa na mahusiano yasiyo thabiti kati ya serikali yake na taifa hilo

https://p.dw.com/p/4S9Ju
USA Washington Außenminister Antony Blinken
Picha: Mandel Ngan/AFP

Safari ya Blinken ya Juni 6-8 inakuja huku Marekani na Saudi Arabia zikijaribu kusuluhisha usitishaji vita wa kudumu kati ya majenerali wanaopigana Sudan.

Wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani imesema katika ziara hiyo, Blinken  atafanya majidiliano kuhusu ushirikiano wa kimkakati wa Marekani na Saudi. Majadiliano hayo yatajikita katika masuala ya kikanda, na masuala mbalimbali ya nchi mbili ikiwa ni pamoja na ushirikiano wa kiuchumi na usalama.

Safari ya Blinken inafuatia ziara ya hivi karibuni kuelekea taifa hilohilo iliyofanywa na mshauri wa Usalama wa Kitaifa wa Ikulu ya Marekani, Jake Sullivan. Pia, ni karibu mwaka mmoja baada ya Rais Joe Biden kuzuru nchi hiyo, huku kukiwa na mafanikio tofauti katika kuboresha uhusiano wa mataifa hayo mawili. Saudia imekuwa mshirika wa Marekani wa muda mrefu Mashariki ya Kati.