1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Blinken ahimiza kufufua uhusiano kati ya Israel na Saudi

6 Juni 2023

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametoa wito wa kufufua mahusiano kati ya Saudi Arabia na Israel, akisema kuwa hilo ni kwa faida pia ya usalama wa taifa la Marekan

https://p.dw.com/p/4SEuO
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken Picha: Hanna Johre/NTB/REUTERS

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken ametoa wito wa kufufua mahusiano kati ya Saudi Arabia na Israel, akisema kuwa hilo ni kwa faida pia ya usalama wa taifa la Marekani. Blinken anatarajiwa leo jioni kuwasili mjini Jeddah na baadaye kuelekea Riyadh ambako atafanya mazungumzo na viongozi wa serikali ya Saudia hususan Mwanamfalme Mohammed bin Salman na viongozi wengine wa Mataifa ya Ghuba. Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani ameendelea kusema kuwa utawala wa rais Biden unafahamu kuwa zoezi hilo la kusawazisha mahusiano kati ya Israel na Saudia ni gumu lakini wamejitolea kufikia lengo hilo. Licha ya uhusiano wa karibu wa muda mrefu, Marekani na Saudia wamepitia misukosuko ya hapa na pale kutokana na masuala ya haki za binaadamu, masuala ya kidiplomasia na kichumi.