1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Benzema kuhamia Saudi Arabia?

Bruce Amani
5 Juni 2023

Je, Mashariki ya Kati huenda ndio inageuka kuwa msakani ya wachezaji mastaa wanaokaribia kukamilisha taaluma zao katika vilabu vya Ulaya? Au ni juhudi za wadau wa eneo hilo kuimarisha na kukuza kandanda?

https://p.dw.com/p/4SCrR
UEFA Champions League Real Madrid v Manchester City
Picha: Juan Medina/REUTERS

Luka Modric na Hugo Loris wako kwenye orodha ya Zaidi ya wachezaji kumi wa ngazi ya juu wanaowindwa na Saudi Arabia katika dirisha hili la uhamisho, wakiongozwa na Lionel Messi na Karim Benzema.

Chanzo kilicho karibu na mazungumzo hayo kimeliambia shirika la Habari la AFP kuwa Sergio Ramos, Jordi Alaba, Sergio Busquets, N'Golo Kante, Angel Di Maria na Roberto Firmino pia ni miongoni mwa washindi wa Kombe la Dunia la Ligi ya Mabingwa wanaowindwa kujiunga na Ligi Kuu ya Kandanda ya Saudi Pro League.

Taarifa hiyo inajiri wakati maafisa wa Saudia wakiwa mjini Paris na Madrid kujaribu kuzinasa Saini za Messi na Benzema kwa mujibu wa ripoti, ambazo zitawawawezesha kujiunga na Cristiano Ronaldo katika taifa hilo la Kifalme lenye utajiri wa mafuta.

Ibahimovic atundika daluga kandanda la kulipwa

Zlatan Ibrahimovic amehitimisha taaluma yake ndefu iliyojaa mataji chungu nzima baada ya kutangaza jana kustaafu kandanda la kulipwa. Mshambuliaji huyo mkongwe alifichua uamuzi wake wa kutundika daluga katika dimba la San Siro baada ya mechi ya mwisho wa msimu ambayo AC Milan ilishinda 3 -1 dhidi ya Verona.

Takwimu kumhusu Zlatan ambaye sasa ana umri wa miaka 41

Magoli 511 ya vilabu
mechi 988 katika taaluma yake

Mfungaji bora wa muda wote Sweden akiwa na mabao 62
Bingwa wa Serie A mara tano

Bingwa wa Ligue 1 mara moja

Bingwa wa Ligi ya Uholanzi – Eredivisie mara mbili

Bingwa wa La Liga mara moja

Bingwa wa Europa League mara moja

afp/reuters/dpa/ap