1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaIsrael

Schumer: Netanyahu amepoteza mwelekeo na kikwazo cha amani

Lilian Mtono
15 Machi 2024

Kiongozi wa walio wengi katika Bunge la Seneti nchini Marekani Chuck Schumer amesema anaamini Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amepoteza mwelekeo.

https://p.dw.com/p/4dXMN
Marekani | Chuck Schumer
Kiongozi wa walio wengi kwenye bunge la Seneti nchini Marekani Chuck Schumer akizungumza na waandishi wa habari katika jengo la bunge Novemba 15, 2023Picha: Anna Moneymaker/Getty Images

Schumer, ambaye ni afisa wa kwanza wa ngazi za juu zaidi nchini Marekani, mwenye asili ya Uyahudi amemkosoa vikali Netanyahu katika hotuba yake ya dakika 40, mapema jana Alhamisi.

Amesema ingawa ana mapenzi na Israel, lakini hatua ya Netanyahu ya kuunda serikali na vyama vya mrengo mkali wa kulia na imemsukuma kukubali kuwaumiza watu wa Gaza na kwa upande mwingine upoteza kwa kiasi kikubwa uungwaji mkono wa kimataifa.

Ingawa amekiri kitisho kikubwa kinachoikabili Israel, lakini amesema watu wa Gaza hawastahili kuteseka kutokana na makosa ya Hamas na Israel na Marekani wanawajibika kimaadili kuwalinda raia.